Connect with us

Makala

Ibenge Awapigia Saluti Simba sc

Licha ya kuambulia sare katika mchezo wa kirafiki kati ya Al Hilal na Simba sc kocha wa klabu ya Al Hilal Frolent Ibenge amewapigia saluti wachezaji wa klabu hiyo kutokana na kiwango kikubwa walichoonesha katika mchezo huo hasa kipindi cha pili na kuwapa kipimo sahihi walichotarajia.

Klabu hizo zilikutana siku ya jumapili katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa kujiandaa na michezo ya kimataifa ambapo Al Hilal iliweka kambi fupi nchini na kucheza mechi za kirafiki dhidi ya Simba sc,Azam FC na Namungo fc ambapo ilishindi mbili na kutoa sare dhidi ya Simba sc.

Al Hilal ilikua ya kwanza kupata bao dakika ya saba likifungwa na Makabi Glody Lilepo ambapo kipindi cha pili Simba sc ilisawazisha kupitia kwa Habib Kyombo na mpaka dakika 90 mchezo uliisha kwa sare ya 1-1.

Katika mahojiano na waandishi wa habari kocha Frolent Ibenge alionyesha kufurahishwa na mchezo huo akisema “Simba wakati wa kipindi cha kwanza sikuwaelewa kwa maana nilitarajia watakuja kwa kushambulia lakini wakaanza na kikosi cha tofauti huku mimi nikianza kwa kujilinda zaidi kipindi cha pili walibadilika tena hasa baada ya kuingiza wachezaji mahiri zaidi”.

Simba sc itaanzia ugenini dhidi ya Horoya Fc ya nchini Guinnea kuanza kutafuta alama zaidi za kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika kutokea kundi C lenye timu hizo pamoja na Vipers na Raja Cassablanca.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala