Connect with us

Makala

Hii Corona Ni Shidaa!!!

Uongozi wa klabu ya Jkt Tanzania  leo Machi 18,2020 umevunja kambi yake kutokana na maelekezo yaliyotolewa jana na Serikali kupitia kwa waziri mkuu Kasim Majaliwa kuhusu zuio la kuwepo kwa mikusanyiko mbalimbali kutokana na kuwepo ugonjwa wa Virusi vya Corona hapa nchini.

Taarifa iliyotolewa na ofisa habari wa Jkt Tanzania , Jamila Mutabazi imeeleza kuwa wachezaji wote wanarejea nyumbani kuanzia leo.

Wachezaji wote wametakiwa kuendelea kujikinga na kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali sambamba na wataalam wa afya ili kuweza kupambana na virusi hivyo vya Corona.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala