Connect with us

Makala

“Hatuwaogopi Yanga sc”-Kaze

Kocha mkuu wa Namungo Fc,Cedric Kaze amesema licha ya Yanga Sc kuwa kwenye kiwango bora ila yeye kama mkuu wa benchi ya ufundi hawaogopi Yanga Sc huku akitanabaisha kuwa anawajua vizuri na wao leo watajitoa katika mchezo wanavyoweza kwenda kupata matokeo ambayo ni bora kwa upande wao .

Kaze ambaye alikua kocha msaidizi wa Yanga sc msimu uliopita ametoa kauli hiyo kuelekea mchezo wa ligi kuu baina ya klabu hizo utakaofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es salaam ambapo Yanga sc watakua wenyeji wa mchezo huo.

“Unajua Yanga Sc wanao timu bora lakini sisi Namungo Fc tumepanga kujitoa Leo”Alisema Kaze wakati akiongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo.

“Tupo tayari kucheza na Yanga Sc na tumeandaa kitu maalumu kucheza na Yanga Sc ,na kiukweli hatuwaogopi Yanga Sc walakusema kuwa tunahofu bali tutakachoenda kufanya leo ni kujitoa ili Namungo Fc ipate Ushindi”

Namungo Fc inapaswa wawe makini katika mchezo huo kutokana na kasi ya Yanga sc ambao katika ligi kuu wakiwa tayari wameshinda michezo miwili kwa idadi ya mabao 10 kwa jumla.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala