Klabu ya Simba Sc kupitia kwa meneja wa Idara ya habari na mawasiliano ya klabu hiyo leo imetangaza kauli mbiu ya mchezo ujao wa nusu fainali dhidi ya Fc Stelleboch ya nchini Afrika ya kusini utakaofanyika Jumapili April 20 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Idara hiyo Ahmed Ally alisema kuwa kauli mbiu ya mchezo huo ni “Hatuishii hapa”.

“Kaulimbiu ya kuingia nusu ilikuwa HII TUNAVUKA na tukafanikiwa lakini kuelekea fainali tunakuja na HATUISHII HAPA. Tunatoka hatua hii tunakwenda fainali. Malengo yetu ni kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.”Alisema Ahmed Ally mbele ya waandishi wa habari
“Kila mtu ni siri yake anajua alifanya nini Simba kufika nusu fainali. Wachezaji wanajua walipambana vipi Simba inafika nusu fainali, viongozi wanajua walipambana vipi, benchi la ufundi wanajua walitumia mikakati gani. Rai yangu kila alichofanya mtu kuipeleka nusu fainali kwenye mechi hii ya kuipeleka fainali basi azidishe mara tatu yake.”Aliendelea kusema.
“Inawezekana sana Simba kucheza fainali sababu ubora huo tunao na kila kitu kimekaa vizuri. Na bahati nzuri fainali tutaanzia ugenini na kumalizia nyumbani. Tushindwe nini? Haleluya.” Alimalizia kisema msemaji Ahmed Ally akiongea na wanahabari visiwani Zanzibar mapema hii leo.
Simba sc itakua na kibarua kigumu zaidi katika mchezo wa nusu fainali kutokana na kutochezea katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambao umefungiwa ambapo watachezea katika uwanja wa New Amaan complex kisha watasafiri kuelekea Afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano.