Connect with us

Makala

Hapatoshi Yanga Sc Ikiwavaa Mc Algers

Jumamosi Januari 18 itakua siku maalumu kwa mashabiki wa Klabu ya Yanga Sc kutokana na timu hiyo kuwania tiketi ya kufuzu robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika itakapovaana na Mc Algers katika michezo ya mwisho ya kundi A la michuano hiyo.

Yanga sc ili ifuzu robo fainali lazima ipate alama tatu katika mchezo huo vinginevyo basi moja kwa moja itakua imetolewa katika michuano hiyo.

 

Tayari klabu hiyo imeanza zoezi la kuuza tiketi za mchezo huo ambapo mpaka sasa mashabiki wameshaanza kuzinunua kwa wingi.

“Niwapongeze sana Mashabiki na Wanachama wa Klabu yetu kwa Kujitokeza mapema kununua tiketi za mchezo wetu dhidi ya MC Alger kabla ya kutangaziwa kwenye Mkutano na Wanahabari”,Alisema Ally Kamwe mkuu wa idara ya habari ya klabu ya Yanga sc.

“Niwapongeze mashabiki na wanachama wa Yanga Sc,Tiketi nyingi tayari zimeisha kabla hata mkutano wa hamasa au klabu kutangaza rasmi uuzwaji wa tiketi, mwamko wa Wanayanga umekuwa mkubwa sana,wananchi wameingia wenyewe kwenye mfumo wa N-Card na kununua tiketi bila klabu kutangaza chochote. Wananchi wameonesha kwa vitendo kwa kiasi gani wanaitaka mechi, VIP A tayar zimeisha”,Alimalizia kusema Kamwe

Yanga sc imeamua kushusha bei ya tiketi hizo ambapo kiingilio cha chini ni shilingi elfu tatu za kitanzania huku kiingilio cha juu ikiwa na shilingi elfu thelasini tu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala