Aliyekua kocha wa klabu ya Yanga sc Miguel Gamondi mapema leo ameondoka nchini kuelekea nyumbani kwao nchini Argentina kwa mapumziko mafupi huku akisubiri kukamilisha dili la kujiunga na moja ya klabu ya Kaskazini mwa bara la Afrika.
Kocha huyo aliyechukua nafasi ya kocha Nasredine Nabi katika klabu ya Yanga sc alitimuliwa klabuni hapo wiki chache zilizopita na mabosi wa klabu hiyo kutokana na kiwango duni cha mastaa wake hali iliyopelekea kupoteza michezo miwili dhidi ya Azam Fc na Tabora United.
Licha ya kutimuliwa bado kocha huyo aliendelea kusalia nchini ambapo inasemekana alikua na mazungumzo na klabu ya Singida Black Stars ambao wamemsimamisha kocha Patrick Aussems kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa kikosi hicho ambacho hakijapata ushindi katika michezo mitatu mfululizo.
Inasemekana mazungumzo ya Gamondi na mabosi wa Singida Black Stars hayakuzaa matunda huku dau la mshahara likiwa kikwazo kikubwa kwa mabosi hao.
Baada ya dili hilo kushindikana moja kwa moja kocha huyo ameondoka nchini akirudi nyumbani kwa ajili ya mapumziko mafupi na akisikilizia ofa mbalimbali alizonazo mkononi kutoka nchini za kiarabu Afrika pamoja na ofa kadhaa kutoka Afrika ya kusini.
Katika Picha alizoweka katika mtandao wake wa kijamii wa instagram imeonyesha akiwa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akijiandaa kusafiri kurudi nchini kwao.