Connect with us

Makala

Gadiel Afungiwa

Beki wa kushoto wa Simba, Gadiel Michael amefungiwa mechi tatu na faini ya 500,000/= kwa kosa la kuingia uwanjani masaa sita kabla ya mchezo wa dhidi ya Mbeya City kisha akaenda kumwagia vitu venye asili ya unga unga katikati mwa uwanja.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi, nyota huyo aliambatana na watu kadhaa waliyovalia nguo zenye nembo ya Simba ambapo licha ya Walinzi kuwazuia walilazimisha mpaka adhma yao kutimia masaa machache kabla ya mchezo baina ya klabu hiyo na Mbeya City Fc ambao uliisha kwa sare ya 1-1.

Pamoja na kupewa adhabu hiyo pia klabu ya Mbeya City nayo imetozwa faini ya kiasi cha shilingi laki tano baada ya viongozi wa klabu hiyo kulazimisha kuingia uwanjani wakati mahojiano baina ya Azam Tv na makocha yakiendelea uwanjani huku pia waamuzi wa mchezo huo wamepelekwa katika kamati ya maadili kutokana na uamuzi mbovu katika kutafasiri baadhi ya sheria.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala