Connect with us

Makala

Zahera Ala Shavu Polisi Tanzania

Kocha wa zamani wa klabu ya Yanga sc Mwinyi Zahera amekamilisha dili la kujiunga na klabu ya Polisi Tanzania kwa mkataba wa miezi sita mpaka mwishoni mwa msimu huu wa ligi kuu nchini.

Tayari kocha huyo ameshafikia makubaliano na kusaini dili hilo huku akisubiri kutambulishwa mbele ya wachezaji wa klabu hiyo akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Joslin Bipfubusa raia wa Burundi ambaye mkataba wake ulisitishwa Oktoba 26, 2022 kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo, miezi mitatu tangu ajiunge nayo Julai 26.

Mkurugenzi huyo wa zamani wa soka la vijana katika klabu ya Yanga sc anatarajiwa kuongeza ufanisi katika kikosi cha timu hiyo ambacho kimecheza mechi tisa za ligi kuu ikiambulia pointi tano tu baada ya kushinda moja, sare mbili na kufungwa sita, hali iliyosababishwa kocha mkuu  kutimuliwa hasa baada ya kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Tanzania Prisons.

Tayari klabu hiyo imeshatoa taarifa kwa umma kufikia makubaliano na kocha huyo mwenye kupenda soka safi la kushambulia na kuzuia ikibidi akiwa na uzoefu wa kuitumikia mpaka timu ya taifa ya Congo Drc kama kocha msaidizi mara kadhaa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala