Connect with us

Makala

Feisal,Aucho Kuivaa Namungo Fc

Kikosi kamili cha klabu ya Yanga sc sasa kimerejea baada ya kocha msaidizi Cedrick Kaze kutangaza kwamba mastaa Khalid Aucho na Feisal Salum wanarejea kuivaa Namungo katika mchezo wa ligi kuu nchini utakaofanyika kesho katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mastaa hao wanarejea baada ya kuwa na majeraha walipojitonesha wakiwa katika majukumu ya timu za Taifa na kusababisha kukosekana uwanjani kwa kipindi cha wiki kadhaa huku wakikosa michezo muhimu kama dhidi ya Azam Fc na Geita Gold ambapo Yanga sc iliteseka kupata ushindi.

Kaze ambaye ni kocha msaidizi wa klabu hiyo amebainisha wakati akizungumza na waandishi wa habari kwamba Aucho na Feisal wanaungana na Chico Ushindi na Farid Mussa kuongeza nguvu katika kikosi hicho huku akijinasibu kuwa watapata alama tatu dhidi ya Namungo ambayo haijafungwa na Yanga sc tangu ipande ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala