Kiungo Feisal Salum ameifungia klabu yake ya Yanga sc bao pekee katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya timu ya Kmc uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam na kuifanya klabu hiyo ikae kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini.
kocha Nasredine Nabi ambaye anakabiliwa na presha kubwa hasa kutoka kwa waandishi wa habari kutokana na mwenendo wa timu hiyo hasa baada ya kutolewa katika michuano ya kimataifa na Al Hilal alilazimika kuwatumia Heritier Makambo,Gael Bigirimana na Ibrahim Bacca ambao mara nyingi hukaa benchi kutokana na kuwakosa baadhi ya nyota akiwemo Fiston Mayele,Benard Morrison na Feisal Salum kutokana na sababu mbalimbali.
Kmc ambayo iko katika kiwango kizuri katika siku za karibuni chini ya mwalimu Thierry Hitimana ilianza mpira kwa kasi huku ikishambulia na kukaba kwa nidhamu kubwa chini ya Baraka Majogoro aliyefanya kazi kubwa kumzuia Stephane Aziz Ki ambapo Matheo Anthony alikosa mabao kadhaa ya wazi.
Kipindi cha pili kocha Nabi alifanya mabadiliko ya kiufundi akimtoa nahodha Bakari Mwamnyeto,Tuisila Kisinda na Dickson Ambundo na kuwapa nafasi Feisal Salum,Zawadi Mauya na Jesus Moloko ambapo dakika ya 80 Feisal aliipatia bao kwa pasi ya Aziz Ki.
Kutokana na ushindi huo sasa Yanga sc imefikisha alama 17 katika michezo saba ya ligi kuu nchini ambapo Mtibwa Sugar wapo nafasi ya pili na alama katika michezo tisa na Simba sc wakiwa nafasi ya tatu na alama 14 katika michezo sita ya ligi kuu.