Connect with us

Makala

Fainali FA Kupigwa Arusha Julai 2

Shirikisho la soka (TFF)nchini limetangaza kuwa fainali ya michuano ya kombe la shirikisho la Azam Sports zitafanyika jijini Arusha Julai 2 mwaka huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini humo.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo kutoka Tff inaonyesha kwamba nusu fainali zitapigwa jijini Mwanza na Arusha katika uwanja wa Ccm Kirumba na Sheikh Amri Abeid  ambapo zitawakutanisha Yanga sc dhidi ya Simba sc siku ya Mei 28 mchezo utakaoanza saa tisa na nusu alasiri huku mchezo wa pili kati ya Azam Fc dhidi ya Coastal Union ukifanyika jijini Arusha katika uwanja tajwa.

Mpaka sasa Simba sc ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo wakiwa wamewafunga Yanga sc katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma mwaka jana ambapo Simba sc alishinda bao 1-0 lililofungwa na Thaddeo Lwanga.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala