Connect with us

Makala

Dodoma jiji Yaomba Kuahirishwa Mnyama

Klabu ya soka ya Dodoma Jiji FC imeandika barua kwa bodi ya ligi [TPLB] kuomba mchezo wao dhidi ya Simba SC usogezwe mbele kutokana na baadhi ya mastaa wa klabu hiyo kuwa na majeraha.

Hii ni baada ya kupata ajali siku ya Jumatatu na wachezaji wao nane (8) kuumia na kushonwa nyuzi wakati wakitoka Ruangwa mkoani Mtwara kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc.

Basi la klabu hiyo likiwa na mastaa wa klabu hiyo lilidumbukia mtoni na baadhi ya mastaa kuumia na kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Mchezo huo ulipaswa uchezwe Februari 15 katika uwanja wa KMC Complex ambapo tayari klabu hiyo imeuandikia barua uongozi wa bodi ya ligi kuu ikiomba mchezo huo usogezwe mbele ili mastaa wa klabu hiyo wakae sawa kiafya na kisaikolojia.

Katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini Dodoma Jiji ipo nafasi ya 11 ikiwa na alama 20 katika michezo 18 ya ligi kuu iliyocheza mpaka sasa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala