Connect with us

Makala

Daktari Afunguka Jeraha la Inonga

Daktari wa klabu ya Simba sc Edwin Kagabo amefunguka kuhusu jeraha alilolipata beki Henock Inonga baada ya kukanyagwa vibaya na mshambuliaji Hija Ugando wa Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu uliozikutanisha timu hizo katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Inonga alipata majeraha yaho mapema kipindi cha kwanza ambapo alipatiwa matibabu uwanjani na baada ya kupata matibabu haraka alipelekwa hospitali kwa matibabu zaidi na uchunguzi wa kina wa jeraha hilo.

Daktari wa timu hiyo Edwin Kagabo amesema Inonga alichanika juu kidogo ya kifundo cha mguu na ameshonwa nyuzi 13 katika jeraha hilo na tayari ameruhisiwa kurudi nyumbani.

Daktari huyo pia  amesema kurejea uwanjani kwa Henock kunategemea na namna kidonda kitakavyopona mapema, kwani ameumia eneo ambalo aliumia katika mchezo wa msimu uliopita dhidi ya Tanzania Prisons.

Msimu huu umekua mbaya kwa beki huyo kwa maana ya amekua akiumia mara kwa mara ambapo alikosa mechi za mwanzoni mwa msimu baada ya kuumia bega katika mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate Fc ambapo alikaa nje ya uwanja kwa takribani wiki mbili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala