Connect with us

Makala

Coastal Union Yafufukia Mkwakwani

Klabu ya Coastal Union hatimaye baada ya michezo mingi ya ligi kuu ya Nbc nchini leo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Singida Black Stars.

 

Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ambao ulikua umefungwa kwa muda mrefu ukifanyiwa ukarabati umeshuhudiwa matokeo ambayo hayakutarajiwa na wengi kutokana na ubora wa Singida Black Stars.

Coastal union ilianza kupata bao dakika ya 47 ya mchezo baada ya Arthur Badda kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa mpira wa faulo iliyopigwa golini mwake na Lucas Kikoti lakini Jonathan Sowah alisawazisha bao hilo kwa penati baada ya kuangushwa na kipa wa Coastal Union katika eneo la hatari dakika ya 76 ya mchezo na kufikisha mabao 9 katika ligi kuu ya Nbc nchini.

Wakati watu wengi wakitarajia Singida Black Stars kufanya “Comeback” ya nguvu mambo yalibadilika dakika ya 82 ya mchezo baada ya Coastal Union kufanya shambulizi la ghafla na kupata bao kupitia kwa Bakari Msimu.

Singida Black Stars baada ya sare hiyo wamekosa nafasi ya kupanda mpaka nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu ambapo sasa wamesalia katika nafasi ya nne na alama 50 katika michezo 26 ya ligi kuu ya Nbc nchini huku Coastal Union wakipanda mpaka nafasi ya 10 na alama 28 katika michezo 26 ya ligi kuu ya Nbc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala