Connect with us

Makala

Chama,Mugalu,Morrison Kuwakosa Asec

Keulekea Mchezo wa siku ya Jumapili wa kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Klabu ya Asec Mimosa Klabu ya Simba imetangaza kuwa itawakosa wachezaji wake Chris Mugalu ambaye amevunjika mkono, Kibu Denis Majeruhi ,Clatous Chama , Thadeo Lwanga majeruhi na Bernard Morrison aliye simamishwa

Kikosi hicho tayari kipo katika maandalizi ya mwisho ya mchezo huo huku nyota hao wakithibitishwa kukosekana katika mchezo huku ikitajwa kwamba tayari Kibu Dennis ameanza mazoezi taratibu na anatarajiwa kupatikana katika michezo ijayo.

Simba sc inakabiliwa na ratiba ngumu ya michuano ya kimataifa ikiwa na michezo takribani mitatu katika muda wa wiki mbili ambapo itacheza na Asec Mimosa siku ya Februari 13 nyumbani kisha itasafiri kuwavaa USGN februari 19 na baadae kucheza na Rs Berkane Februari 23.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala