Connect with us

Makala

”Tunaonewa” Yanga sc Walalamika

Klabu ya Yanga sc imelalamika kutotendewa haki na waamuzi wa ligi kuu nchini kiasi cha kusababisha kuwa na matukio mengi tata katika michezo inayowahusisha wao nchini.

Yanga sc kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari Hassan Bumbuli na Haji Manara wamefanya mkutano na waandishi wa habari kulalamika kuhusu uonevu huo ikiwemo kunyimwa nafasi za kufunga kwa kisingizio cha Offside pamoja na kupunjwa dakika za nyongeza baada ya dakika tisini za mchezo.

“Kumekuwa na mlolongo wa matukio ya maamuzi yenye utata ambayo kwa namna moja au nyingine yananyima haki ya timu zingine na yanatoa manufaa Kwa timu zingine,”Tunataka Waamuzi wetu waanze kujitafakari juu ya haya ambayo yamekuwa yakiendelea na yamekuwa mjadala mkubwa sana kwenye Taifa letu, Lakini pia tunataja mamlaka zinazosimamia mpira zichukue hatua juu ya jambo hili ambalo watu wamewekeza pesa zao”Alisema Bumbuli.

“Kuna matukio karibu 10 yanayohusisha Simba ambayo Watu wamelaumu na hatua hazijachukuliwa, hatuna shida ya neno tulizolizoea la kusadikika Waamuzi nao ni Binadamu hatuna shida ila hilo la Ubinadamu liwe pande zote”.Alisema Haji Manara ambaye ni Afisa Habari klabuni hapo.
“Mechi na Biashara, Beki wa Simba kafanya mchezo wa hatari kabisa, nani alichukuliwa hatua!?, Mechi mmoja Golikipa wao alifanya mambo ya ajabu kabisa lakini hakuchukuliwa hatua, unawezaje kuchukua hatua tukio la Polisi ukaacha tukio la Biashara”Aliendelea kusema.
Bumbuli pia aliitaka kamati inayosimamia waamuzi nchini ijitafakari na kuchukua hatua kuhusu maamuzi mabovu ya waamuzi hao.
“Tunaisihi kamati ya waamuzi kutafakari yale yanayoitwa makosa ya kibinadamu ambayo yamekuwa yakizinufaisha timu fulani fulani na nyingine zikiumia. Kwahiyo kamati ya waamuzi na waamuzi wake wajitafakari,” Mkuu wa Habari Yanga sc Hassan Bumbuli alizidi kutiririka zaidi.
Yanga sc ipo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini ikiwa na alama 36 huku Simba sc ikifuatia kwa alama 31 ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala