Connect with us

Makala

Chama Aipasua Kichwa Simba sc

Mabosi wa klabu ya Simba sc wanakuna kichwa jinsi ya kumuongezea mkataba kiungo Cletous Chama ambae mkataba wake wa miezi 12 unaelekea katikati ambapo kufikia mwezi januari anaruhusiwa kuanza mazungumzo na klabu yeyote kisheria.

Chama alijiunga na Simba sc akitokea klabu ya Rs Berkane baada ya kushindwa kupata nafasi na kujikuta akiozea benchi na kuamua kuvunja mkataba na kujiunga na Simba sc kwa mkataba wa mwaka mmoja ambao utafika ukingoni mwishoni mwa msimu huu wa ligi kuu nchini.

Kinachowaumiza kichwa mabosi wa Simba sc ni juu ya gharama za kumuongezea mkataba huo wa miaka miwili ambao takribani zaidi ya shilingi milioni 150 zinahitajika ili kumshawishi staa huyo kusalia klabuni hapo na dau hilo linaweza kuongezeka kutokana na umuhimu wake kikosini humo akiwa tayari ameshasaidia upatikanaji wa mabao saba akifunga moja na kusaidia sita.

Chama amekua na mchango mkubwa klabuni hapo tangu ajiunge nayo akitokea Rs Berkane ambapo inasemekana alikua na majeraha hali iliyosababisha mabosi hao kumpa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwingine.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala