Taarifa kutoka kwa mabosi wa klabu ya Yanga sc zinasema kuwa mshambuliaji Clement Mzize anahitajika nchini Ubelgiji ambapo kuna offa mpya ya takribani bilioni mbili na nusu imewasili.
Awali Mzize alikua akihitajika na vilabu vya Kaskazini mwa bara la Afrika ingawa klabu yake imekua ikiweka ngumu kumuachia kutokakana na kuendelea kuhitaji huduma yake kikosini humo.
Klabu za Wydad Athletic ya nchini Morocco sambamba na baadhi ya vilabu vingine nchini humo vimewasilisha ofa nyakati ambazo mara nyingi hufikia kati ya bilioni moja na nusu kitu ambacho klabu yake haitaki kumuachia kutokana na bei hizo kuwa ndogo.
Kubwa kuliko sasa ni ofa hiyo mpya ambayo imewachanganya mabosi wa klabu hiyo kutokana na fedha nyingi za usajili huku kikwazo kikiwa ni ugumu wa kumuachia kwani anahitajika mwezi huu Januari.
“Ni kwa sababu tu wiki hii hajacheza lakini tayari ungesikia kuwa kuna offa mpya kwani hivi sasa kuna ofa kutoka ubelgiji bilioni mbili na nusu tukiachana na offa za Kaskazini”,Alisema bosi mkubwa klabuni hapo.
Mzize amekua na kiwango kizuri tangu kuwasili kwa kocha Sead Ramovic ambapo amekua mwiba kwa mabeki wa timu pinzani kutokana na kasi yake akifunga na kuassisti mabao.
Mpaka ligi kuu inasimama tayari staa huyo amefikisha mabao sita katika msimamo wa wafungaji katika ligi kuu nchini.