Connect with us

Makala

Bangala,Djuma Wapo Sana Yanga sc

Klabu ya soka ya Yanga sc imefanikiwa kuwaongeza mikataba mipya nyota wawili wa klabu hiyo Djuma Shabani na Yannick Bangala ambayo sasa itaisha mwaka  2025 baada ya jana kusaini mikataba hiyo mbele ya uongozi wa Yanga sc akiwemo Rais wa klabu hiyo Eng.Hersi Said na wakala wa wachezaji hao Faustin Mkandila.

Awali Djuma na Bangala walijiunga na klabu hiyo wakitokea As Vita Club ya nchini Congo huku Bangala akitokea nchini Algeria ambako alivunja mkataba wake na kuja kujiunga na klabu ya Yanga sc ambapo msimu huu amefanikiwa kupata tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu nchini.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani za klabu ya Yanga sc tayari sasa iko kwenye mazungumzo na mshambuliaji Fiston Mayele ili nae aongeze mkataba mpya baada ya kuwepo na ofa nyingi kutoka nje ya nchi.

Yanga sc inajiimarisha zaidi ndani ya uwanja ili kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa ambapo ina miaka mingi haijafanya vizuri kama mahasimu wao Simba sc na tayari imefanikiwa kuwanasa baadhi ya wachezaji kama Lazarus Kambole,Benard Morrison,Joyce Lomalisa na Gael Bigirimana kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala