Connect with us

Makala

Azam Fc Yatua Kwa Mmorocco

Klabu ya Azam Fc ipo mbioni kumalizana  na kocha Rachid Taoussi raia wa Morroco kuja kuifundisha klabu hiyo akichuaa nafasi ya Yousouph Dabo aliyetimuliwa klabuni hapo wiki iliyopita kutokana na mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha licha ya klabu hiyo kufanya usajili mkubwa katika dirisha kubwa la usajili msimu huu.

Dabo alitimuliwa kutokana na kufungwa 4-1 na Yanga sc katika fainali ya michuano ya Ngao ya jamii kisha siku chache baadae akatolewa na Apr ya Rwanda katika hatua ya awali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 ugenini nchini Rwanda na kuhitimisha ndoto za mabosi wa klabu hiyo za kucheza hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika.

Taoussi ambaye amekuwa kocha wa timu za vijana za Morocco kwa miaka kadhaa huku pia akiwa ni Mkurugenzi wa ufundi wa timu ya wakubwa ya nchi hiyo tayari yupo mbioni kumalizana na mabosi wa Azam Fc ambapo mazungumzo yamefika mbali wakikubaliana kuhusu maslahi binafsi sambamba na mambo mengine muhimu.

Awali kabla ya Taoussi,Azam Fc ilianza mazungumzo na kocha wa Al Hilal Fc Florent Ibenge lakini mahitaji makubwa ya kocha huyo yaliwarudisha nyuma huku pia wakijaribu kuulizia upatikanaji wa Juma Mgunda anayeinoa Simba Queens lakini mpaka sasa Taoussi yupo mbioni kukamilisha dili hilo.

Kocha huyo ana uzoefu akizifundisha kabla za Far Rabat,Raja Casablanca,FUS Rabat zote za Morroco kwa mafanikio makubwa akiziwezesha kutwaa mataji mbalimbali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala