Connect with us

Makala

Azam Fc Yaipumilia Simba sc

Ushindi wa mabao 2-1 ilioupata klabu ya Azam Fc dhidi ya Singida Black Stars umeisogeza timu hiyo mpaka nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini ikizidiwa na Simba sc kwa alama moja pekee.

Azam Fc baada ya kushinda mchezo huo imefikisha alama 27 huku Simba sc ikiwa na alama 28 huku Azam Fc ikiwa imecheza michezo 12 na Simba sc ikiwa na michezo 11.

Mabao ya Feisal Salum dakika ya 38 na lile la mshambuliaji raia wa Colombia Jhonier Blanco dakika ya 57 huku Elvis Rupia akifunga bao la kufutia machozi kwa Black Stars dakika ya 62 japo halikuzuia Azam Fc chini ya kocha Rachid Taoussi kuondoka na alama tatu muhimu katika mchezo huo.

Idd Selemani “Nado” aliufanya mchezo huo kuwa mikononi mwake akitoa pasi zote mbili za mabao kwa pasi maridadi hali iliyompa tuzo ya uchezaji bora wa mchezo huo.

Singida Black Stars pamoja na kumsimamisha kocha Patrick Aussems na Dennis Kitambi bado imeendelea kutopata ushindi katika mchezo wa nne mfululizo katika ligi kuu ya Nbc nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala