Connect with us

Makala

Azam Fc Yaifuata Singida Black Stars

Klabu ya Azam Fc imeanza safari mapema ya leo kuifuata Singida Black Stars katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini utakaofanyika kesho jumapili katika uwanja wa Ccm Liti mjini Singida.

Azam Fc baada ya kushinda 3-0 dhidi ya Kengold Fc ilirejea Dar es Salaam na leo alfajiri imeanza safari kwa kutumia treni ya mwendokasi mpaka dodoma kisha itapanda basi moja kwa moja mpaka Singida.

Kocha Rachid Taoussi anatarajiwa kuingiza kikosi chake kamili katika mchezo huo kutokana na kuhitaji kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa ambapo Singida Black Stars ni washindani wakubwa wa nafasi hiyo.

Punde baada ya kupata ushindi dhidi ya Kengold Fc kocha alisema kuwa anahitaji pia kushinda michezo inayofuatia.

“Vijana wanapambana, morali ya ushindi wanayo, lakini hii ni kutokana na ubora na uimara wa timu, niwapongeze lakini tunaenda kujipanga na mechi zinazofuata,” amesema kocha huyo.

Katika msimamo wa ligi kuu mpaka sasa Azam Fc wapo nafasi ya tatu na alama 51 katika michezo 24 huku Singida Black Stars wakiwa nafasi ya nne na alama 47 katika michezo 24.

 

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala