Connect with us

Makala

Azam Fc Basi Tena!

Ndio mchezo umeisha kwa klabu ya Azam Fc baada ya kulazimishwa suluhu na Coastal Union katika uwanja wake wa nyumbani wa Chamazi katika mchezo wa ligi kuu uliomalizika jioni ya leo uwanjani hapo na kufifisha matumaini ya ubingwa wa ligi kuu kwa klabu hiyo tajiri nchini.

Azam Fc kabla ya kucheza mechi hiyo ilikua ngumu kuwatoa katika mbio za ubingwa kutokana na mahesabu lakini kushindwa kuondoka na alama tatu kunafifisha matumaini hayo baada ya kufikisha alama 25 25 katika mchezo wa 16 na kuendelea kushika nafasi ya tatu  ikizidiwa pointi sita na mabingwa watetezi Simba sc yenye mechi moja mkononi huku ikiwa nyuma ya Yanga  yenye pointi  42 za mechi 16 pia ambapo ni tofauti ya alama 17.

Tofauti hiyo inamanisha ili Azam Fc awe kileleni ni lazima Yanga sc ipoteze michezo 6 na kutoa sare moja kitu ambacho ni kigumu huku akiiombea Simba sc ipoteze michezo mitatu katika ya 15 huku yenyewe Azam Fc ikishinda michezo yote 14 iliyosalia kwenye ligi kitu ambacho ni kigumu kutokea.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala