Connect with us

Makala

Arjentina Yafuzu Nusu Fainali na Vituko Kibao

Timu ya Taifa ya Argentina imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Uholanzi kwa jumla ya mabao 4-3 baada ya kumaliza dakika 12o kwa kufungana mabao 2-2.

Licha ya kutangulia kufunga mabao mawili kupitia kwa Nahuel Molina 37′ na Lionel Messi 73’kwa mkwaju wa penati Uholanzi ilisawazisha mabao hayo dakika za 83 na dakika 11 za nyongeza kupitia kwa Wout Werghost na kuingia katika changamoto ya mikwaju ya penati ambapo Argentina walishinda na kufuzu nusu fainali.

Licha ya kufuzu hatua hiyo kamati ya nidhamu ya Fifa imeamua kuifungulia mashtaka timu hiyo ya taifa baada ya kuvunja sheria na kanuni za michuano hiyo ambapo refa Antonio Mateu Lahoz alitoa kadi za njano 12 kwa timu hiyo huku Uholanzi wakipata kadi nyekundu ambapo hii ni mara ya pili kwa timu hiyo ya taifa wakirudia ya mwaka 2014.

“Kamati ya nidhamu ya Fifa imefungua mashtaka dhidi ya shirikisho la soka nchini Argentina kutokana na kukiuka kifunga cga 12 kinachihusu mwenendo wa wachezaji na viongozi na kile cha 16 kinanchohusu taratibu na usalama wa mchezo cha kanuni za nidhamu za Fifa katika mchezo dhidi ya Uholanzi siku ya 9/12/2022” Ilisomeka taarifa hiyo ya Fifa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala