Connect with us

Makala

Hapatoshi Ufaransa Vs Morocco Nusu Fainali Wc

Patachimbika ndio neno linalofaa kulitumia kuelekea mchezo wa nusu fainali katika ya Ufaransa na Morocco katika michuano ya kombe la dunia linaloendelea nchini Qatar ambapo wadau wa soka duniani wamekua wakiusubiri kwa hamu mchezo huo.

Morocco imefuzu hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Ureno 1-0 huku Ufaransa ikiifunga Uingereza 2-1 katika michezo ya robo fainali iliyochezwa wikiendi iliyopita.

Ufaransa atakua na kazi ya ziada kuifungua safu ya ulinzi ya Morocco ambayo imefanikiwa kutoruhusu magoli katika michezo dhidi ya Hispania na Ureno na kuwa timu ya kwanza barani Afrika kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa duniani.

Mashabiki wengi wa nchi za kiarabu na Afrika watagawanyika katika kushabikia timu hizo kwa sababu Ufaransa ina raia wengi kutoka nchi za Afrika Magharibi ikiwemo Morocco,Algeria pamoja na nchi za kiafrika zinazozungumza kifaransa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala