Connect with us

Soka

Yanga sc Yatua Mwanza

Kikosi cha klabu ya Yanga sc mapema asubuhi ya leo kimeondoka jijini Dar es salaam na kutua jijini Mwanza kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold Fc utakaofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini humo siku ya Jumapili.

Yanga sc imewasili Mwanza ikiwa na mastaa wake wote wa kikosi hicho waliofiti huku ikifurahia urejeo wa Feisal Salum aliyekua amefungiwa mchezo mmoja pamoja na Dickson Job ambaye alikua na adhabu ya kukosa michezo mitatu pia winga Chico Ushindi ambaye amerejea kutoka katika majeraha.

Yanga sc inahitaji kushinda mchezo huo ili kujiwekea mazingira mazuri ya kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini ambapo mpaka sasa inaongoza ikiwa na alama 42 katika michezo 16.

Yanga sc inatakiwa ijipange hasa ili kuifunga Geita Gold sc kutokana na timu hiyo kuwa na wachezaji walioichezea Yanga sc kwa vipindi tofauti wakiwemo Kelvin Yondani,Juma Mahadhi,Maka Edward pamoja na Adeyun Salehe ambao watahitaji kuwaonyesha waajiri wao wa zamani kuwa walikosea kuwatema.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka