Connect with us

Makala

Genk Yampandisha Kelvin John

Klabu ya Krc Genk imethibitisha kuwa Kelvin John amepandishwa kwenye timu ya wakubwa hivyo atacheza michezo ya ligi kuu nchini Ubelgiji akitokea timu ya watoto ya klabu hiyo.

Kinda huyo Mtanzania alisaini kujiunga na klabu hiyo mwezi june mwaka jana akisaini mkataba wa miaka mitatu ambapo atakaa hapo mpaka mwaka 2024 akiwa ni Mtanzania wa pili kuichezea klabu hiyo akitanguliwa na Mbwana Samata ambaye aliuzwa kwenda Aston Villa.

Kelvin John ni mshambuliaji wa kitanzania anayetegemewa kufanya makubwa katika medani za kimataifa ambapo pia anaichezea timu ya Taifa ya Tanzania ya wakubwa(Taifa Stars) lengo likiwa ni kumpa uzoefu zaidi.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala