Connect with us

Soka

Stars yangara ugenini kufuzu Qatar 2022

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Benin ugenini katika harakati zake za kufuzu kombe la dunia 2022 nchini Qatar katika mchezo wa kundi J.

Simon Msuva aliipatia Tanzania bao pekee la mchezo dakika ya 6 kwa shuti kali lililotinga wavuni mara baada ya kuwachambua walinzi wa Benin katika dimba la

Stars sasa wamefikisha pointi saba katika michezo minne ya kundi hilo na kukaa kileleni kwa tofauti ya magoli ya kufunga kabla ya mchezo mwingine wa kundi hilo kati ya DR Congo na Madagascar.

Kocha wa Taifa Stars alifanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi chake kwa kuwaanzisha mlinzi wa kati Kennedy Juma na mshambuliaji Kibu Denis wakichukua nafasi za John Bocco na Mzamiru Yassini.

Tanzania imebakiza michezo miwili pekee kwenye hatua za makundi dhidi ya DR Congo nyumbani na Madagascar ugenini na endapo watamaliza kinara wa kundi lao basi watasonga katika hatua inayofuata ya mtoano inayohusisha mataifa 10 yaliyomaliza kileleni mwa makundi yao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka