Connect with us

Soka

Twiga Stars mabingwa COSAFA 2021

Timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu ‘Twiga Stars’ wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa COSAFA upande wa wanawake kwa mwaka nchini Afrika Kusini baada ya kuwafunga Malawi 1-0 katika mchezo wa fainali.

Twiga Stars ilijipatia goli lake la ushindi dakika ya 64 kupitia kwa Enekia Kasonga bao pekee la mchezo huo,ikumbukwe kuwa Twiga Stars ni waalikwa kwenye michuano hiyo inayohusisha mataifa yanayopatikana ukanda wa Kusini mwa Afrika maarufu kama COSAFA.

Nahodha wa timu hiyo Amina Bilal ametwaa tuzo binafsi ya mchezaji bora wa mashindano hayo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu kupitia kurasa zake rasmi wa Instagram na twitter ameipongeza timu hiyo kwa kuliletea Taifa heshima kwa kutwaa kombe hilo.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka