Connect with us

Makala

Simba Sc Yafuzu Nusu Fainali Crdb

Ushindi wa mabao 2-1 ilioupata klabu ya Simba Sc dhidi ya Klabu ya Bigman Fc umeivusha moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Crdb nchini.

Simba sc ilipata Ushindi huo jioni ya leo katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam na kuvuka hatua hiyo.

Kocha Fadlu Davis alimuanzisha kipa Hussein Abel huku mabeki wa kati wakicheza Duchu sambamba na Hussein Kazi na safu ya ushambuliaji iliongozwa na Lionel Ateba.

Joshua Mutale leo aliifungia Simba sc bao la kwanza dakika ya 15 ya mchezo akiunganisha pasi ya Valentino Nouma aliyecheza upande wa kushoto na kuipatia Simba sc bao la uongozi.

Dakika ya 30 ya mchezo huo Lionel Ateba aliifungia Simba sc bao la pili kwa penati baada ya beki wa Bigman Fc kumuangusha Ellie Mpanzu katika eneo la hatari.

Kipindi cha kwanza Joseph Henock aliipa bao la kifutia machozi klabu yake ya Bigman akifunga bao kwa shuti kali lililomshinda kipa Hussein Abel dakika ya 44 ya mchezo.

Mpaka dakika 90 zinakamilika Simba sc ilikata tiketi ya kufuzu hatua inayofuatia huku Bigman Fc ikiaga mashindano moja kwa moja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala