Connect with us

Makala

Injinia Atua Burundi Kukamilisha Usajili

Taarifa kutoka nchini Burundi zinasema klabu ya  Yanga sc  ipo katika hatua za mwisho kumalizana na winga wa nchi hiyo Jean Claude Girumugisha ambaye anakipiga katika klabu ya Al Hilal O.SC inayonolewa na kocha Florent Ibenge.

Winga huyo amewavutia vigogo hao wa soka nchini Tanznia kupitia mashindano ya klabu bingwa Afrika ambapo Yanga sc walikutana nae mara mbili katika michezo ya hatua ya makundi.

Rais wa klabu hiyo Eng.Hersi Said siku chache zilizopita hakuwepo nchini inatajwa kuwa kuna wachezaji kadhaa anaenda kufanya nao mazungumzo kwenye kipindi hiki ligi zimesimama.

Hata hivyo klabu hiyo italazimika kutoa fungu kubwa kumsajili winga huyo kutokana na kuwa na mkataba ulio hai na klabu yake ya Al Hilal  Fc.

Winga huyo mwenye miaka 20 ya kuzaliwa alijiunga na klabu ya Al Hilal akitokea klabu ya Magara Young Boys mwaka 2023.

Katika michuano ya ligi ya klabu bingwa barani Afrika msimu huu mpaka sasa winga huyo amefunga mabao matatu katika michezo tisa aliyoichezea klabu yake.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala