Connect with us

Makala

“Uwanja Upo Tayari”Msigwa Awaita Caf

Msemaji mkuu wa Serikali na Katibu mkuu wa Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mh.Gerson Msigwa amesema uwanja wa Benjamin Mkapa uko tayari kwa ukaguzi wa wa Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) hata leo au kesho wala sio tarehe 20 March, 2025, waliosema wao.

Msigwa amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari na maelezo ambapo amesema ameshangaa kuona CAF wanasema kiwanja kibovu na kimefungiwa kwa muda ilihali kiwanja kiko sawa na kiko tayari kwa ukaguzi.

“Eneo la kuchezea liko vizuri sana kama linavyoonekana kwenye picha mnato na mjongeo ambazo mmeziona hivi punde”,Alisema Msigwa.

“Labda kama kuna jambo lingine nje na hili, vinginevyo Simba Sc watacheza Benjamin Mkapa mchezo wao wa Robo Fainali kwani kiwanja hakina shida yoyote”,Aliendelea kusema mbele ya waandishi wa habari.

“Tumeleta mashine mpya mbalimbali kama unavyoziona kwenye picha na zinafanya kazi nzuri sana na kiwanja kiko na standard bora sana. Mustafa mtu wa CAF wa viwanja siku zote tuko nae na hivi sasa ameenda kwao kwajili ya mfungo, lakini tunafanya naye kazi vizuri sana, bega kwa bega, kila anachoelekeza kinafanyiwa kazi”.

Msimamo wa Serikali mpaka sasa ni kuwa uwanja upo tayari huku ikiwataka Caf kuja kuugagua hata sasa kwani kila kitu kipo tayari kama ambavyo walielekeza.

Hatari kubwa inayohofiwa ni kuwa mchezo baina ya Simba Sc dhidi ya Al Masry unaweza usifanyike uwanjani hapo endapo Caf wataona kuwa uwanja huo una kasoro.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala