Connect with us

Makala

Dube Mchezaji Bora Februari 2025

Kamati maalumu ya usimamizi wa ligi kuu ya Nbc nchini imemchagua mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Prince Mpumelelo Dube kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari nchini aliwazidi Selemani Bwenzi wa Kengold Fc pamoja na Stephan Aziz Ki.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Bodi ya Ligi kuu nchini imesema kuwa mshambuliaji huyo amepata tuzo kutokana na kuwa na mchango mkubwa katika michezo ambayo klabu yake imecheza mwezi Februari.

Dube amepata tuzo hiyo baada ya kufunga mabao matano na kutoa asisti tano katika michezo saba ya ligi kuu iliyocheza klabu yake ya Yanga sc kwa mwezi huo.

Dube aliongoza Yanga sc katika suluhu dhidi ya Jkt Tanzania huku wakiifunga Singida Black Stars 2-0,Kmc 6-1 Mashujaa 5-0 huku pia wakiifunga Pamba Jiji Fc mabao 3-0 ugenini jijini Mwanza.

Pia walizifunga Kengold 5-1 pamoja na Kagera Sugar 4-0 na kuipaisha Yanga sc kileleni mwa ligi kuu ya Nbc nchini.

Mpaka sasa katika msimamo wa wafungaji Dube ana mabao 10 katika msimamo huo huku pia akiwa amesaidia upatikanaji wa mabao saba mpaka sasa.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala