Connect with us

Makala

TFF Yapiga Nyundo Viwanja Vitatu

Shirikisho la soka nchini imeamua kuvifungia viwanja vya CCM Kirumba,Jamhuri Pamoja na CCM Liti uliopo mjini Singida kutokana na kuwa na miundombinu iliyochakaa kwa mujibu wa kanuni na leseni za ligi kuu nchini kuhusu viwanja vya michezo ya ligi kuu ya Nbc.

Taarifa za kufungiwa kwa viwanja hivyo vinavyotumiwa na timu za Pamba Jiji,Singida Black Stars Pamoja na Dodoma jiji Fc ambapo sasa vilabu hivyo vinapaswa kutafuta viwanja vingine kwa ajili ya michezo yao ya ligi kuu.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la soka nchini (TFF) imesema kuwa miundmbinu ya viwanja hivyo haijakidhi matakwa ya kanuni kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya Kanuni na leseni za klabu za ligi kuu ya Nbc nchini.

Timu za Singida Black Stars,Pamba Jiji Fc,Dodoma Jiji Pamoja na Tabora United sasa zinapaswa kutafuta viwanja vingine kwa ajili ya michezo yao ya nyumbani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala