Connect with us

Makala

Medo Ajiunga na Singida Black Stars

Aliyekua kocha wa klabu ya Kagera Sugar Fc Mellis Medo amejiunga na klabu ya Singida Black Stars mara baada ya kuachana na klabu ya Kagera Sugar kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

Medo alijunga na klabu hiyo akitokea Mtibwa Sugar lakini sasa klabu hiyo imeamua kuachana nae kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi hicho ambacho sasa kinashika nafasi ya pili kutoka mkiani kikiwa na alama 15 tu katika michezo 21 ya ligi kuu ya Nbc nchini.

Punde tu baada ya kuachana nae tayari klabu ya Singida Black Stars imeamua kumuajiri kocha huyo kama kocha msaidizi huku pia wakimpa kazi ya kulishauri benchi la ufundi la klabu hiyo.

Medo raia wa Marekani atashirikiana na makocha David Ouma ambaye ndie kocha mkuu sambamba na Juan Magro na Muhibu Kanu.

Katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini Singida Black Stars mpaka sasa ipo katika nafasi ya nne  ikiwa na alama 38 katika michezo 21 ya ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala