Connect with us

Makala

Simba Sc Vs Azam Fc Kupigwa Benjamin Mkapa

Bodi ya ligi kuu nchini imetoa taarifa za kuuhamishia mchezo baina ya Simba sc dhidi ya Azam Fc katika uwanja wa Benjamin Mkapa badala ya Azam Complex Chamazi ulikopangwa kufanyika awali.

Mchezo huo unaofanyika leo jumatatu February 24 umehamishwa ili kutoa nafasi kwa mashabiki wa soka nchini kuhudhuria kwa wingi ambapo pia muda wa mchezo huo umesogezwa mpaka saa moja jioni badala ya saa 10 jioni iliyopangwa kufanyika awali ili kutoa nafasi kwa mashabiki ambao watakua makazini na kwenye shughuli mbalimbali.

Uwanja wa Benjamin Mkapa una uwezo wa kuchukua mashabiki takribani elfu sitini waliokaa huku ukiwa na taa ambazo zinaruhusu kuchezeka kwa michezo usiku.

Awali uwanja huo ulikua unatumika kama uwanja wa nyumbani kwa timu za Simba sc na Yanga sc lakini Wizara ya Sanaa,Michezo na Utamaduni uliamua kusitisha matumizi ya uwanja huo ya mara kwa mara ili kufanya ukarabati mkubwa kwa ajili ya mashindano ya mataifa ya Afrika ambayo yatafanyika mwaka 2027 katika nchi za Tanzania,Kenya na Uganda.

Simba sc na Azam Fc unatarajiwa kuwa mchezo mgumu kwani kila timu inahitaji alama tatu ili kusogea juu ya msimamo wa ligi kuu ambapo mpaka sasa Simba sc ina alama 50 katika nafasi ya pili ikicheza michezo 19 huku Azam Fc ikiwa na alama 43 katika michezo 20 ya ligi kuu ya Nbc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala