Connect with us

Makala

Fedha Kuamua Hatma ya Ngoma Simba Sc

Wakala wa kiungo wa klabu ya Simba Sc Fabrice Ngoma Airways Faustine Mkandila amesema kuwa fedha ndio kitu ambacho kitaamua hatma ya kiungo huyo klabbuni hapo akielekea kumaliza mkataba wake msimu huu.

Wakala huyo amethibitisha kuwa mchezaji huyo anaelekea mwishoni mwa mkataba wake huku tayari akiwa na ofa kadhaa kutoka nje ya Tanzania.

Mkandila amesema kuwa kwa sasa wanasubiri amalize mkataba wake na klabu hiyo ili wafanye maamuzi ya wapi ataelekea huku fedha ndio itaamua zaidi kuhusu uelekea huo.

“Hakuna chochote kilichofanyika kati yetu na Simba wala timu nyingine. Kwa sasa mchezaji yupo na Simba Sc na ibakie kuwa hivyo, lakini kama ataondoka au atabaki ni suala muda sahihi ukifika uamuzi utafanyika”,Alisema Mkandila

“Hakuna mazungumzo yoyote yanayoendelea baina yetu na Simba au klabu nyingine. Mchezaji kwa sasa yupo kwenye klabu yake na kumbuka kuwa kinachohitajika ni fedha. Hawa wachezaji wanacheza kwa ajili ya kutafuta fedha, hivyo inapokuja ofa nzuri ataipa kipaumbele,” alimalizia Kusema Mukandila.

Ngoma msimu huu anamaliza mkataba wake klabuni hapo lakini kuna dalili kubwa ya kubaki kutokana na kocha Fadlu Davis kuonyesha imani kubwa akimtumia kila mchezo huku akimpa nafasi ya kuwa nahodha msaidizi wa kikosi hicho.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala