Connect with us

Makala

Simba Sc Yarejea Kileleni Kwa Kishindo

Klabu ya Simba Sc imefanikiwa kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex Jijini Dar es Salaam.

Ikitoka kupoteza alama mbili katika mchezo uliopita dhidi ya Fountain Gate Fc,Simba Sc ilifanya mashambulizi makali na kufanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya 28 ya mchezo likifungwa na Jean Charles Ahoua akipokea pasi ya Kapombe.

Simba Sc iliendeleza mashambulizi makali na hatimaye Ellie Mpanzu alifunga bao la pili kwa Simba Sc na la kwanza kwake tangu asajiliwe kikosini humo akipigia shuti kali baada ya kupokea pasi ya Lionel Ateba dakika ya 45 kipindi cha kwanza.

Dakika moja mbele Ladack Chasambi alifunga bao la tatu kwa Simba sc akipokea pasi nzuri ya Kapombe na kuamsha shangwe uwanjani hapo.

Mapumziko Simba sc ilikua inaongoza mabao 3-0 dhidi ya wajelajela ambapo kipindi cha pili hakukua na upande uliopata bao.

Simba imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini ikifikisha alama 47 huku katika michezo 18 ya ligi kuu huku Tanzania Prisons ikiwa mkiani mwa ligi nafasi ya 14 na alama 17 katika michezo 18.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala