Connect with us

Makala

Kaseke Aimaliza Azam FC

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga sc Deus Kaseke ameisaidia klabu yake ya Pamba Jiji Fc kuibuka na alama tatu muhimu katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Klabu ya Azam Fc uliofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza.

Kaseke alifunga bao pekee katika mchezo huo muda mchache baada ya kuingia ambapo alikutana na pasi nzuri na kumchungulia kipa Mohamed Mustapha dakika ya 86 ya mchezo huo.

Pamba jiji awali walinyimwa bao la mapema baada ya mwamuzi kudai kuwa mfungaji wa Pamba Jiji alicheza rafu kabla y kufunga bao hilo.

Pamba Jiji sasa baada ya kuchukua alama tatu mbele ya Azam Fc wamefikisha alama 18 katika nafasi ya 12 ya ligi kuu ya Nbc wakicheza michezo 18 ya ligi kuu.

Kamati ya hamasa ya klabu hiyo iliyopo chini ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Said Mtanda awali iliahidi kuwakabidhi wachezaji wa timu shilingi milioni 15 kama bonasi ya kupata ushindi lakini jioni mkuu huyo wa mkoa alipandisha zawadi hiyo mpaka milioni 30 za kitanzania ambazo zimekabidhiwa mapema asubuhi ya leo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala