Connect with us

Makala

Ramovic Asepa Yanga Sc

Klabu ya Yanga sc imetangaza kuachana na kocha wake Sead Ramovic kwa makubaliano ya pande zote mbili baada ya kuafikiana kuvunja mkataba wa kocha huyo aliyedumu takribani miezi mitatu klabuni hapo.

Taarifa iliyotolewa na idara ya habari ya klabu hiyo imesema kuwa katika mchezo wa kesho wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Kengold Fc timu hiyo itakua chini ya kocha msaidizi Abdulhamid Moalin.

Ramovic anaondoka pamoja na kocha msaidizi Mustafa Kodro ambapo taarifa za chini ya kapeti zinasema kuwa kocha huyo amepata ofa nono katika klabu ya Cr Belouzdad ya nchini Algeria.

Tayari klabu hiyo imetangaza kocha wa klabu ya Singida Black Stars Miloud Hamdi kuchukua nafasi ya Ramovic klabuni hapo.

Miloud ambaye amejiunga na Singida Black Stars lakini bado hajafanikiwa kukaa benchi hata mechi moja tangu ajiunge na timu hiyo ambapo ameishia kuinoa timu hiyo kambini jijini Arusha tu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala