Connect with us

Makala

Morrison Bado Sana

Pamoja na shauku ya mashabiki wa klabu ya Kengold Fc kumuona uwanjani mshambuliaji wao mpya Bernard Morrison itawalazimu kusubiri kwa muda kutokana na staa huyo kutokua fiti kutumika katika michezo ya ligi kuu nchini.

Punde tu baada ya kusajiliwa kocha wa timu hiyo Vladislav Heric aliamuru staa huyo kupewa mazoezi maalumu ili kurejesha utimamu wake kutokana na kutoka kufanyiwa upasuaji wa goti mwaka jana.

Daktari wa klabu hiyo Amina Turusa alikiri kukosekana kwa Morrison katika michezo ya mwanzoni ambapo bado anaendelea kuwekwa sawa.

Taarifa kutoka ndani ya idara ya habari ya klabu hiyo imeshindwa kuthibitisha suala hilo kwa undani zaidi.

“Mambo mengine ni ya ndani na nisingependa kuyaweka wazi, itoshe kusema ni kweli anaendelea na mazoezi binafsi na suala la yeye kucheza au kutocheza dhidi ya Yanga, hilo litabakia maamuzi ya benchi la ufundi ila nyota wetu wote wako fiti.”Alisema Joseph Mkoko afisa habari wa klabu hiyo.

KenGold inayoburuza mkiani na pointi sita tu katika michezo 16 iliyocheza, itacheza dhidi ya Yanga Jumatano ya Februari 5, kwenye Uwanja wa KMC Complex, huku ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa mechi ya kwanza bao 1-0, Septemba 25, mwaka jana.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala