Kikosi cha Yanga sc kimerejea kwa kishindo katika michuano ya ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kuifunga timu ya Kagera Sugar Fc kwa mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Kocha Sead Ramovic hakua na mabadiliko makubwa kikosini humo ambapo kwa mara ya kwanza alimuanzisha beki Israel Mwenda kama winga wa kulia huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Prince dube sambamba na Clement Mzize na Stephan Aziz Ki.
Eneo la kiungo lilisalia kwa Khalid Aucho na Mudathir Yahaya huku Ibrahim Bacca na Dickson Job wakiwa mabeki wa kati wakisaidiwa na Djigui Diarra na Kibwana Shomari sambamba na Chadrack Boka upande wa kushoto.
Clement Mzize ndie alifungua kalamu ya mabao dakika ya 32 alipomtungua kipa Ramadhani Chalamanda kwa shuti kali huku Mudathir Yahaya akifunga bao la pili dakika ya 60.
Pacome Zouzoua alifunga bao la tatu kwa penati safi baada ya Maxi Nzengeli kuangushwa wakati akijipanga kuzuia mpira ndani ya eneo la boxi huku Kennedy Musonda akifunga bao la nne kwa kichwa safi dakika ya 86 ya mchezo.
kutokana na kupata ushindi huo sasa Yanga sc imefikisha alama 42 katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini na itakutana na Kengold Fc siku ya Jumatano Februari 5 2024.