Connect with us

Makala

Singida Black Stars Yavunja Kambi Arusha

Klabu ya soka ya Singida Black Stars imevunja rasmi kambi yake ya mafunzo iliyofanyika kwa wiki tatu jijini Arusha iliyokua na lengo la kuingiza mbinu mpya za mafunzo kwa mastaa hao.

Mabosi wa klabu hiyo waliamua kuweka kambi hiyo maalumu baada ya ligi kuu ya Nbc nchini kusimama kwa takribani mwezi mmoja ili kupisha michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) ambayo ilipangwa kufanyika hapa nchini kabla ya kughairishwa.

Pia kambi hiyo ililenga kuingiza mbinu za mwalimu mpya Hamdi Miloud ambaye amejiunga na timu hiyo siku za karibuni baada ya kutimuliwa kocha Patrick Aussems.

Katika kambi hiyo timu hiyo ilicheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Mbuni Fc waliyoshinda 4-0 na dhidi ya TMA waliyoshinda 2-1.

Kambi hiyo itarejea mjini Singida ili kuwakaribisha Kagera Sugar Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc Februari 7 kisha kusafiri mpaka jijini Dar es Salaam kuwavaa Kmc Februari 10.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala