Connect with us

Makala

Singida Black Stars Yasajili Aliyewatesa Simba Sc

Klabu ya Singida Black Stars ya mkoani Singida imetangaza kumsajili winga Serge Pokou raia wa Ivory Coast kutokea Al Hilal Omdurman ya nchini Sudan.

Nyota huyo moja kati ya wachezaji waliowindwa sana na Simba Sc kipindi cha dirisha kubwa wakati akiwa ASEC Mimosas lakini akaamua kuelekea Al Hilal kutokana na kuvutiwa na nguvu ya usajili wa waarabu hao.

Hata hivyo staa huyo amekua hapati nafasi ya kuanza kikosini mara kwa mara huku akitokea benchi mara kadhaa katika kikosi cha kocha Florent Ibenge.

Usajili wa mshambuliaji huyo ulikamilika dakika za mwisho za kufungwa kwa dirisha la usajili jana Januari 15 2024 na sasa staa huyo muda si mrefu atawasili jijini Arusha katika kambi ya mafunzo ya klabu hiyo.

Pokue amefunga Simba sc mara kadhaa anapokutana nao tangu alipokua na Asec Mimosa mpaka alipotua Al Hilal Omdurman.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala