Connect with us

Makala

Bangala Atemwa Azam Fc

Mabosi wa klabu ya Azam Fc wamefikia uamuzi wa kuachana na mchezaji kiraka Yanick Bangala kwa makubaliano ya pande zote mbili ili kupisha ingizo jipya kikosini humo.

Bangala aliyesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kununuliwa chini ya kocha Yousouph Dabo kutoka Yanga sc amekubaliana na mabosi wa klabu hiyo kuvunja mkataba wake wa miezi nane uliosalia.

Mabosi wa Azam Fc ili kuepuka kufungiwa na Fifa kuhusu masuala ya usajili wameamua kumlipa mshahara yake yote iliyosalia kama gharama ya kuvunja mkataba huo ambapo sasa nafasi yake itachukuliwa na mshambuliaji Allasane Diao aliyekua majeruhi.

Kocha Rachid Taoussi ameonekana kukubaliana na kiwango cha Allasane Diao na kuamuru arudishwe kwenye mfumo wa usajili klabuni hapo na beki huyo kuondolewa rasmi.

Tayari mchezaji huyo ameshapokea rasmi taarifa hiyo na sasa anaaglngalia ofa zingine ndani na nje ya Tanzania.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala