Connect with us

Soka

Che Malone Awazawadia Pamba Fc Beki katili

Beki wa klabu ya Simba Sc Che Malone Fondoh pamoja na mshambuliaji wa klabu hiyo Lionel Ateba wameizawadia klabu ya Pamba Jiji Fc beki Cherif Ibrahim aliyejiunga na klabu hiyo msimu huu wa dirisha dogo la usajili.

Beki huyo amejiunga na Pamba jiji akitokea klabu ya nyumbani kwao Cameroon ya Cotton Sports Fc ambapo ametua pamba kws mkataba wa miezi sita pekee.

Cherif amesema kwamba sababu kubwa ya kutua Pamba Jiji Fc ni ushauri aliopewa na mastaa hao wa klabu ya Simba Sc ambapo moja kwa moja aliukubali baada ya kumuelezea kuhusu uzuri na ushindani uliopo katika ligi kuu nchini.

“Nilikuwa na mazungumzo na Che Malone na Leonel Ateba kuhusu ligi ya Tanzania. Che Malone aliniambia mambo mazuri sana kuhusu soka la hapa, akasisitiza ubora wa wachezaji na mazingira ya ligi. Alinifundisha kuhusu ushindani mkubwa wa Ligi Kuu Bara na kwamba ni fursa nzuri kwa mchezaji kama mimi, ambaye ninataka kuonyesha uwezo wangu,” alisema Ibrahim ambaye ni beki wa kushoto

Baada tu ya kumuona uwanjani kocha Fred Felix Minziro alikubaliana na uwezo wa beki huyo na moja kwa moja kuagiza asajiliwe klabuni hapo.

“Cherif ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa, ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi mbalimbali uwanjani. Alipokuja kwetu, alileta ari na hamu ya kushinda. Hili ni jambo muhimu,” alisema.

Pamba Jiji Fc inafanya usajili kabambe wa dirisha dogo ili kuepuka kushuka daraja ambapo mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini ipo nafasi ya 13 ya msimamo ikiwa na alama 12 ikicheza jumla ya michezo 15.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka