Connect with us

Makala

Chirwa,Sey Kuiokoa Kengold Fc

Washambuliaji Obrey Chirwa na Stephen Sey wapo katika hatua za mwisho kujiunga na timu ya Kengold Fc ili kuinusuru na kushuka daraja katika ligi kuu ya Nbc nchini.

Kengold Fc ipo mkiani mwa ligi kuu ambapo ili kujinusuru mabosi wa timu hiyo wamepanga kuwatema mastaa takribani 13 kisha kusajili wapya.

Chirwa anakamilisha taratibu za kuhama kwa mkopo kutoka Kagera Sugar Fc huku Sey akikamilisha mazungumzo ya kujiunga na klabu hiyo baada ya kuwa huru tangu aachane na klabu ya Anwar Al-Abyar ya Libya.

Sambamba na sajili hizo pia kocha mkuu wa Kengold Fc Omary Kapilima anahitaji pia kukamilisha baadhi ya sajili kama Lassa Gradi Kiala ambaye ni kiungo mshambuliaji wa zamani wa klabu ya St.Eloi Lupopo ya nchini Drc.

Pia klabu hiyo inaangalia uwezekano wa kumsajili Benard Morrison japo kuna utata kuhusu mshahara ambapo staa huyo anahitaji kiasi cha shilingi milioni kumi kwa mwezi ili aweze kusaini timu hiyo.

Klabu hiyo mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu nchini ina alama sita pekee katika michezo 15.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala