Connect with us

Makala

Coastal Union Yaendelea na Safisha Safisha

Baada ya kuachana na Kipa wake Raia wa Congo Dr Ley Matampi sasa klabu hiyo imetangaza kuachana na beki wake Hernest Malonga pamoja na Deus Lucas baada ya kuvunja mkataba wake klabuni hapo.

Malonga mchezaji wa zamani wa klabu ya Ihefu Fc ambayo sasa ni Singida Black Stars anaondoka klabuni hapo kwa makubaliano na uongozi wa Klabu hiyo kuvunja mkataba huo.

Pia uongozi wa klabu hiyo chini ya kocha Juma Mwambusi umeendelea na kusafisha kikosi hicho ili kuruhusu kufanya sajili mpya zenye tija kikosini humo.

Mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini Coastal Union ina alama 16 katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu ikiwa imecheza michezo 13 tu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala