Connect with us

Makala

Manula Abaki Airport Dar

Taarifa mpya kutoka ndani ya klabu ya Simba Sc ni kuwa kipa Aishi Manula amebaki nchini mara baada ya kupata matatizo ya kiafya akiwa katika uwanja wa ndege wa Mwl.Nyerere jijini Dar es Salaam wakati kikosi cha timu hiyo kikipaa kuelekea nchini Algeria kuvaana na klabu ya Fc Constantine katika mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika.

Awali katika orodha iliyotolewa ya mastaa wa klabu hiyo watakaosafiri kuelekea nchini humo jina la Manula lilikuwemo ambapo staa huyo aliugua ghafla baada ya kufika uwanja wa ndege dakika chache kabla ya kuanza safari.

Taarifa rasmi iliyotolewa na klabu hiyo imesema kuwa kipa huyo sasa amebaki nchini kutokana na Changamoto hiyo na kufanya Simba sc kusafiri na makipa wawili pekee ambao ni Moussa Camara na Ally Salim.

Simba sc itavaana na Fc Constantine ya nchini humo siku ya Jumapili ikiwa ni mchezo wa pili kwa timu hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 katika mchezo wa awali dhidi ya Onze Bravos ya Msumbiji.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala