Connect with us

Makala

Aussems,Kitambi Wasimamishwa Singida Bss

Klabu ya Singida Black Stars imewasimamisha makocha wake Patrick Aussems ambaye ni kocha mkuu sambamba na msaidizi wake Dennis Kitambi kutokana na mwenendo usioridhisha wa kikosi hicho katika michuano ya ligi kuu ya Nbc nchini.

Kikosi hicho licha ya kuwa katika nafasi ya nne ya msimamo kikiwa na alama 24 katika michezo 11 ya ligi kuu nchini hakijapata ushindi katika michezo yake mitatu ya ligi kuu mfululizo ikichota alama mbili pekee kati ya alama tisa.

Michezo hiyo mitatu iliyosababishwa kusimishwa kwa makocha hao ni suluhu dhidi ya Coastal Union kisha kupoteza kwa 1-0 dhidi ya Yanga sc Visiwani Zanzibar na kisha sare ya 2-2 dhidi ya Tabora United.

Tayari klabu hiyo imetoa taarifa kwa umma kupitia vyanzo vyake rasmi kuhusu suala hilo ambapo sasa timu hiyo itakua chini ya Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo Ramadhan Nswanzurimo na kocha msaidizi atakua Muhibu Kanu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala